Tuesday, October 18, 2016
Kama wewe ni mtunzaji misitu au mazingira hii inaweza kukuhusu
http://i0.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2016/10/IMG-20161018-WA0022.jpg?resize=660%2C400
Kwa muda mrefu tumekuwa na kampeni nyingi za kuhamasishana kuhusu upandaji miti au utunzaji misitu na wapo baadhi ya watu wetu ambao walishawahi kufikiwa na zawadi kuhusiana na issue ya Mazingira kwenye list yako ya watu waliopata zawadi kutokana na mazingira inabidi uwaongeze wananchi wa Kijiji cha Katurukila Morogoro.
img-20161018-wa0020
Nimeipata ya Waziri wa Mazingira na Muungano ofisi ya Makamu wa Rais,January Makamba ameahidi kutoa mifuko 100 ya saruji kwa kijiji cha Katurukila wilaya ya Kilombero Morogoro, kama kutambua mchango wao mkubwa katika utunzaji wa mazingira hasa eneo la Msitu wa Magombera.
img-20161018-wa0026
Miongoni mwa maeneo ya Kilombero ambayo January Makamba ameyatembelea ni pamoja, Kilosa kwenye Mto Mkondoa, Kilombero, Msitu wa Magombera,Kijiji cha Kiturukila na Mto Lumemo Ifakara, kuhusu mgogoro wa msitu wa Magombera kati ya wanakijiji na mwekezaji Ramadhan Rashid Kuhuka, Waziri Makamba amesema kuwa tayari kesi imeshafika mahakamani na ni busara kuiachia mahakama.



0 comments:
Post a Comment