Wednesday, February 15, 2017
Waamuzi Yanga na Ngaya wawekwa hadharani
Mchezo wa marudiano ya Ligi ya Mabingwa ya Afrika kati ya Young Africans ya Tanzania na Ngaya ya Comoro kwenye hatua ya awali utachezeshwa na Waamuzi kutoka Uganda.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), waamuzi hao ni Alex Muhabi Nsulumbi atakayepuliza filimbi uwanjani.
Nsulumbi atasaidiwa na Ronald Kakenya na Lee Okello wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Brian Nsubuga Miro huku Kamishna akitokea Afrika Kusini ambaye ni Monnyenyone Lucas Nhlapo.
Mchezo huo utafanyika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kama ambavyo Young Africans walithibitisha CAF majuma mawili yaliyopita kabla ya tarehe ya mchezo huo ambayo ni Februari 18, mwaka huu.



0 comments:
Post a Comment