Propela

aa

million ads

Millionaire  Ads

Wednesday, February 15, 2017

PICHA: Wachezaji wa Bongo walivyoonesha #mapenzimubashara siku ya Valentine

kwa watu wao wa karibu. Mapenzi ni kitu cha ajabu, wapo wanaoweza kuamini ni bahari kwa sababu hayana mwisho na yanabeba visafi kwa vichafu, vibovu na vinavyovutia, vibaya kwa vizuri na pengine baraka au mikosi. Mapenzi huanza na mahusiano na yapo kila sehemu kuanzia chini ya paa za nyumba njiani kuelekea makazini mpaka kwenye nyumba za ibada. Kwa sababu upendo ni maisha, basi upendo ni michezo pia. Wanamichezo wanahusudiwa kwa kazi za miguu na mikono yao pia, lakini hata nyoyo zao kuna wakati hufanya kazi zaidi ya kusukuma damu yaani hukiuka misingi aliyoisema msanii maarufu Ditto. Kuna wakati wachezaji huonekana kama ni wahuni na makatili kutokana na kile wanachokifanya wakati wanapotimiza majukumu yao viwanjani lakini nihawa pia ambao huonekana malaika kwa wapenzi wao au wenza wao. Leo nakupa list ya baadhi ya wachezaji wa kibongo ambao waliitumia siku ya wapendanao kuonesha upendo kwa watu wao wa karibu kwa ku-post picha picha na kuwatakia kila la heri katika siku hiyo maalum kwa wapendanao.

0 comments:

Post a Comment