Dar es Salaam. Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Tanzania (CDF), Jenerali Venance Salvatory Mabeyo amekula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma, leo (Jumatatu) jijini hapa.
Jenerali Mabeyo amekula kiapo akishuhudiwa na Kamishna wa Maadili wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela.
Wakati huo huo, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Tanzania, Luteni Jenerali James Alois Mwakibolwa pia amekula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma.



0 comments:
Post a Comment