Propela

aa

million ads

Millionaire  Ads

Wednesday, February 1, 2017

Abdi Banda nje kwa siku 10

Klabu ya Simba itamkosa beki wake kisiki, Abdi Banda atakuwa nje kwa siku 10 kwa ajili ya kupumzisha mwili sambamba na kuuguza majeraha yake ya misuli aliyoyapata hivi karibuni. Banda atakosa mchezo ujao wa timu hiyo dhidi ya Majimaji lakini akiaminika kuwa ataweza kucheza mechi dhidi ya Yanga, Februari 25. Banda aliongea na gazeti la Championi amesema “Mimi nipo nyumbani nimepewa siku 10 za kupumzika kwa ajili ya kupoza misuli yangu ambayo ilikaza baada ya kufanya mazoezi magumu kwa miezi miwili mfululizo. “Wakati nikiwa nje ya timu nitakosa mechi hii inayokuja dhidi ya Majimaji na muda wote huo nitakuwa naenda hospitali kwa ajili ya kupatiwa tiba ya tatizo langu,”alisema Banda.

0 comments:

Post a Comment