Monday, January 30, 2017
Waliookolewa mgodini watoka hospitali.
Waliookolewa mgodini watoka hospitali
Monday, January 30, 2017
Geita. Wachimbaji 15 waliokuwa wamelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Geita kwa ajili ya matibabu baada ya kuokolewa katika mgodi wa RZ walikokuwa wamefunikwa na kifusi cha udongo kwa siku tano wameruhusiwa kutoka hospitali baada ya afya zao kuwa nzuri.
Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Brian Mawala amesema afya za wachimbaji hao zimeimarika na wana uwezo wa kuendelea na kazi.
Baada ya kuruhusiwa leo asubuhi wamekutana na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Ezekiel Kyunga.




0 comments:
Post a Comment