Saturday, January 28, 2017
Trump hakutaja 'Wayahudi' katika hotuba yake ya kuadhimisha 'Holokosti'
Trump hakutaja 'Wayahudi' katika hotuba yake ya kuadhimisha 'Holokosti'
Saturday, January 28, 2017
Trump hakutaja 'Wayahudi' katika hotuba yake ya kuadhimisha 'Holokosti'
Katika hotuba yake ya maadhimisho ya mauaji ya wayahudi milioni 6 kipindi cha utawala wa Nazi chini ya uongozi wa Adolf Hitler,rais mpya wa Marekani Donald Trump ametumia neno la 'Waathiriwa wasio na hatia' badala ya kuwatambulisha wayahudi.
"Ni kwa heshima,moyo mzito na huzuni kuu kuwakumbuka mashujaa na waathirika wa mauaji makubwa ya Holokosti.Haiwezekani kufikiria kikamilifu kuhusu unyama uliotendewa watu wasio na hatia katika ugaidi wa Nazi."
Hayo ni maneno aliyotumia bwana Trump katika hotuba yake ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mauaji makuu ya wayahudi.
Hapo miaka ya awali katika hotuba za maraia wa Marekani,walitambulisha waathiriwa kuwa Wayahudi,mwaka jana Barack Obama alitaja Wayahudi mara nne katika hotuba yake ya hafla hiyo.
Shirika kubwa zaidi la kutetea haki za wayahudi Marekani lilishangazwa na tukio hilo na kutuma ujumbe kupitia Twitter kwa White House kuw;
@WhiteHouse Taarifa kuhusu #MaadhimishoyaHolokosti ,White House imeshindwa kutambulisha mauaji ya Wayahudi milioni 6 na kutambulisha kuwa 'watu wasio na hatia'.




0 comments:
Post a Comment