Monday, January 30, 2017
SMZ yafungia kiwanda cha kusindika ngozi
SMZ yafungia kiwanda cha kusindika ngozi
Monday, January 30, 2017
Image result for kiwanda cha kusindika ngozi
Zanzibar. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imekifungia kiwanda cha kusindika ngozi kilichopo Kianga Mkoa wa Mjini Unguja, baada ya kukibaini kuwa kinachangia uharibufu wa mazingira hasa vyanzo vya maji.
Mkuu wa Wilaya ya Magharibi ‘A’ Mwinyiussi Abdalla Hassan, amesema leo (Jumatatu) kuwa wamechukua uamuzi huo baada ya kuona kuwa kiwanda hicho kimeshindwa kufuata taratibu za sheria za uanzishwaji viwanda.
Hassan amesema mmiliki wa kiwanda hicho kabla ya kuanza kazi alitakiwa kufuata sheria za kuhifadhi na kulinda mazingira, ila kutokana na ukaidi wake alifanya kazi zake bila kufuata vigezo stahiki.



0 comments:
Post a Comment