Thursday, January 12, 2017
Rais wa Mexico amjibu Trump
Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto amesisitiza kwa mara nyengine kwamba nchi yake haitalipia ukuta katika mpaka na Marekani.
Ametoa kauli hiyo baada ya Rais mteule wa Marekani, Donald Trump kusema katika mkutano wake na waandishi wa habari kwamba anataka kuanza kuujenga haraka na kwamba Mexico itailipa Marekani kwa gharama iliyoingia.
Bwana Pena Nieto amewaambia wanadiplomasia wa kigeni kwamba yuko tayari kujadili mustakbali wa makubaliano ya kibiashara ya Kaskazini ya Marekani, ambapo Trump amesema hayo ni makubaliano mabaya ya kibiashara kuwahi kupitishwa na Marekani.



0 comments:
Post a Comment