Propela

aa

million ads

Millionaire  Ads

Friday, January 20, 2017

Mvutano wa wafanyabiashara na madalali Arusha washika kasi

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjR4y1QxnM3RqWguQCSSc_bpNkMbVHzBSfZxCh4V8eYv1En5AMS27j2QK6CDRuMR3NwYRJON7VFvkUbBdEOcTCB-VHYup1rBs9Gg5KaeO-rxzYsU93LQKzAayleGDmbv129MG-5-xjxIYo/s400/mpya.png Mvutano kati ya madalali na wafanyabiasha wa jiji la Arusha umechukua sura mpya baada ya zaidi ya wafanyabiashara elfu moja waliyopanga kwenye maduka yanayomilikiwa na jijini la Arusha kwenye eneo la standi ya daladala na soko la Kilombero kuunga mkono hatua ya serikali kuwapa notisi madalali hili kuhakiki upya wapangaji wake kuwa linalengo la kuondoa ukandamizaji na ukwepaji wa kodi wanaofanywa na madalali hao. Wakizungumza kwenye mkutano wa dharura kujadili suala hilo wafanyabiashara wamesema madalali wamekuwa wakilipa kiasi kidogo cha kodi kwa halmashauri na kuwapangisha watu wengine kwa fedha nyingi hivyo hatua ya serikali kutoa notisi kwa madali hili waingie mkataba na wafanyabiashara wenyewe itaondoa ufisadi huo. Akitoa ufafanuzi juu ya mgogoro unaendelea baina ya madalali na wapangishaji katika maduka hayo,Meya wa jiji la Arusha Calisti Lazaro amesema wameamua kuwaondoa madalali hili kudhibiti ukwepaji wa kodi uliyokuwa unaikosesha serkali mapato ya zaidi ya shilingi bilioni mbili kwa mwaka.

0 comments:

Post a Comment