Thursday, January 26, 2017
Moto wa nyika wateketeza mji chile
Mataifa yameanza kutuma wazima moto nchini Chile kusaidia taifa hilo kukabiliana na moto mbaya zaidi katika historia ya taifa hilo.
Urusi imetuma ndege yenye uwezo wa kubeba tani kadha za maji kujaribu kusaidia kuzima moto huo wa nyika.
Kwa Picha: Moto mkubwa watishia Israel
Moto huo umeenea kwa kasi sana maeneo ya kati ya Chile, ambapo unasaidiwa na upepo mkali, kiwango cha juu cha joto na hali kwamba maeneo hayo yamekabiliwa na kiangazi kwa muda.
Mji Santa Olga, unaopatikana kilomita 240 kusini mwa Santiago umeharibiwa kabisa na moto huo.



0 comments:
Post a Comment