Propela

aa

million ads

Millionaire  Ads

Monday, January 23, 2017

Jammeh aiacha hazina ya Gambia tupu, aondoka na mamilioni

Mshauri maalumu wa Rais wa Gambia Adama Barrow amesema zaidi ya dola za Kimarekani milioni 11 zinaaminika kutoweka katika hazina ya serikali, kufuatia kuondoka madarakani kwa mtawala wa muda mrefu Yahya Jammeh. Mia Ahmad Fatty amewaambia Waandishi wa habari katika mji mkuu wa Senegal Dakar kwamba wataalamu wa masuala ya fedha wanatathmini kujua ni kiasi gani kwa sasa kimepotea. Amesema Gambia kwa sasa ina tatizo kubwa kifedha kwa hazina yake kutokuwa na kitu. Lakini mwandishi wa BBC Alastair Leithead anasema maafisa wa Barrow hawajatoa ushahidi wowote kwamba Bw Jammeh aliondoka na pesa hizo.

0 comments:

Post a Comment