Friday, January 27, 2017
Bajeti Ya Halmashauri Ya Wilaya 2016/2017 Imetekelezeka Kwa Asilimia 18
Katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya Kishapu leo hii kabla ya kuanza kuijadili bajeti ya mwaka 2017/2018. Mheshimiwa Diwani wa kata ya Sekebugoro, Ferdinand Mpogomi alitaka kupata ufafanuzi na kujua utekelezaji wa bajeti ya mwaka huu kabla ya kupitisha mpango wa mwaka ujao.
Ndipo Afisa mipango wa halmashauri Mang'era Mang'era akatoa ufafanuzi kuwa, fedha iliyoidhinishwa kwa mwaka wa fedha 2016 /2017 kwa shughuli za maendeleo ni tsh bilioni 14.5 kati ya fedha hizo bilioni 11.01 ni ruzuku kutoka serikali kuu na bilioni 1.7 ni fedha itokanayo na mapato ya ndani na bilioni 1.7 ni fedha za bakaa ya mwaka 2015 /2016. Kwa mujibu wa ufafanuzi huo ndipo akahitimisha kwa kusema kuwa hadi kufikia Desemba 31 2016 halmashauri imetumia jumla ya bilioni 2.7 sawa na asilimia 18 ya bajeti nzima ya miradi ya maendeleo kwa mwaka 2016 /2017.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu mheshimiwa Boniphace Butondo kwa niaba ya baraza alitoa wito kwa serikali kuleta fedha za miradi kwa wakati kwani mpaka sasa bajeti ya 2016 /2017 ilitakiwa iwe imetekelezeka kwa asilimia zaidi ya hamsini kwa sababu hivi sasa tupo katika ya mwaka alisema.
Naye mheshimiwa Ngolomole wa kata ya songwa aliomba serikali kuu itekeleze kwa katika suala zima la utekelezaji wa bajeti kwani ni miaka mitano mfululizo bajeti zimekuwa zikitekelezwa chini ya asilimia hamsini suala ambalo ni kinyume cha matarajio ya bajeti katika kuboresha maisha ya wana Kishapu na watanzania kwa ujumla.



0 comments:
Post a Comment