Propela

aa

million ads

Millionaire  Ads

Thursday, January 12, 2017

Alichokisema Lipumba Morogoro

Morogoro. CUF ndiyo chama cha siasa kinachoweza kupambana na mafisadi, dhuluma na uonevu na siyo vyama vingine. Hiyo ni kauli ya Mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Profesa Ibrahimu Lipumba aliyoitoa kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi wa diwani wa Kata ya Kiwanja cha Ndege mjini Morogoro. Profesa Lipumba amesema CCM na Chadema haviwezi kupambana na ufisadi kwa sababu bado vina baadhi ya viongozi waliowahi kutuhumiwa kuhusishwa na ubadhirifu. Pia, amewataka wakazi wa kata hiyo kumchagua mgombea udiwani kupitia chama hicho, Abeid Mlapakolo ili alete mabadiliko ndani ya kata yao.

0 comments:

Post a Comment